Watu wengi wanapata shida kuwapata madalali wa nyumba sehemu mbali mbali za jiji la Dar es Salaam.
Pamoja ni kuwa madalali wengi wamekuwa siyo waaminifu katika kuwahudumia wateja wa Tanzania real estates kabla hujajua pa kupata huduma tofauti, leo nitakuletea sehemu tatu wanapopatikana madalai wa nyumba Sinza:
Sinza Kumekucha.
Hapa ni sehemu ambapo madalali hukaa chini ya mti wakisubiria wateja. Ukitokea Shekilango uliza Sinza Kumekucha ukishashuka gari muulize mtu yeyote wapi madalai wa nyumba wanapatikana. Atakuonesha mti ambapo wanakuwa wamekaa kusubiri wateja. Ila uwe mwangalifu maana hawan ofisi hivyo unaweza kuingia nao mikataba kama siyo mwanaminifu akapotea usimwone tena.
Sinza Mori.
Sinza Mori ni mbele kidogo ya Sinza Kumekucha. Hapo napo utawakuta madalali wameketi wakisubiri wateja. Usitegemee kuwakuta ofisini na kuona nyumba walizonazo, ila watakutajia maeneo mbali mbali ambapowan nyumba hizo. Si lazima iwe Sinza, ila watakutajia hata kawe, Kinondoni, Mwenge na hata Mbagala. Ni vizuri kuwa makini maana hizo nyumba wanazotaja si kweli kuwa wanazo ila wanategemea madalali wengine kutoka maeneo hayo.
Bamaga
Hapa ni makutano ya kona ya barabara ya Shekilango na ile ya Bagamoyo. Ulizia madalali wa nyumba wanapatikana wapi. Watakueleza sehemu ambapo pia wanakaa kusubiria wateja.
Ili kuepuka matatizo ambayo yanaweza kusababishwa na madalali wasio waaminifu, ni vizuri ukapata madalali wa nyumba ambao wana ofisi na walioshajiriwa na wanaofanya biashara ya Tanzania real estates kwa muujibu wa sheria.
Kwa kupata huduma tofauti katika tanzania real estates njoo Hot Emi Properties ili tukuhudumie.
No comments:
Post a Comment