Thursday, May 24, 2012

Kwa nini utafute Nyumba ya Kupanga Kupitia Hot Emi Properties?

Katika biashara ya tanzania real estates, wapo wengi wanaendelea kuifanya hapa Dar es Salaam na mikoa mingine. Ila cha kushangaza, biashara hii inafanyika siyo kama inavyofanywa katika nchi zingine, kama UK, USA n.k. Hapa kwetu biashara hii imeshikiliwa sana na madalali wa nyumba ambao wamekuwa wakiifanya namna ambavyo watenja wao wamebaki na malalamiko.

Ili kuepuka usumbufu huo, Hot Emi Properties wamekuja na njia sahihi za kufanya biashara ya Tanzania real estates. Hivyo, sababu kuu za kuja kwa Hot Emi Properties ni kama ifuatavyo

          1. Utachagua nyumba, kiwanja au shamba kupitia video. 

Kama ilivyo hivi sasa, madalali wa nyumba huwazungusha mtaa hadi mtaa ili kuwatafutia nyumba wateja. Wakati mwingine, pamoja na juhudi hizo za kuzunguka, huwa nyumba haipatikani na ni lazima mteja atoe pesa ya kuzungusha ambayo ni kati ya sh. 5,000 hadi sh. 10,000. Hii imeleta usumbufu mkubwa sana kwa wateja. Kutatua tatizo hili, Hot Emi Proprties imeanzisha mpango ambapo nyumba za kuuzwa au kupngisha kupigwa picha za video na mnato na kuoneshwa katika ofisi zao. Hii hupunguza muda wa kuzunguka na kwenda kuangalia nyumba mitaani.

2. Shamba au nyumba huhakikiwa na watalaam wa ardhi kutoka wizarani.

Kampuni ya Hot Emi Properties huwatumia watalaam wa ardhi ili kutoa uhalali wa shamba au sehemu inayouzwa ili kuepuka matapeli ambao wamekuwa wakiwaibia wateja kwa kuwauzia sehemu ambazo haziuzwi.

3. Mikataba yote ya ununuzi au kupanga husainiwa mbele ya wanasheria. 

Biashara za Tanzania real estates hakika kuwa utapeli mwingi. Hilo tumeliona na kuamua kuwatumia wanasheria katika maswala ya ardhi ili kusimamia mikataba ambayo tunaingia na wateja wetu ili wasitapaliwe. 

4. Kampuni itahakikisha mteja wake haonewi na mwenye nyumba

Baada ya kuuza au kupangisha nyumba au frem, kampuni hufuatilia kuona kama mteja wetu haonewi na mwenye nyumba. Huduma hii huitwa kitalaam after sale service. Huzikutanisha pande zinazosigana ili kutatua migogoro katika mikataba kama inatokea.

5. Mteja atapata taarifa sahihi za sheria ya makazi na haki zake

Kampuni huwapa wateja wake taarifa sahihi kuhusu sheria na taratibu za makazi na kutoa ushauri namna nzuri ya ununuzi au upangaji wa makazi unaoendana na sheria inavyotaka. 
Karibu Hot Emi Properties ili upate huduma zetu bora

No comments:

Post a Comment