Monday, January 11, 2016

Bomoa Bomoa na Biashara ya Madalali wa Nyumba

Mambo yanayogusa vichwa vya habari hivi karibu hapa Tanzania, ni hatua ya bomoa bomoa ya nyumba zilizojengwa mahali pasipo sitahili. Hatua hii inatekelezwa na Rais wa awamu ya tano Mh. Magufuli. 

Katika makala ya leo tunataka kuangalia ni jinsi gani hatua hii itawahusisha madali wa nyumba na jinsi gani tunaweza kuepuka kutapeliwa kupitia madali wa nyumba wasio waaminifu.

1. Ununuzi wa Viwanja
Mara nyingi watu wamekuwa wakiwatumia wadalali katika kununua viwanja vya ujenzi. Na kwa kuwa madalali wanapenda pesa za haraka haraka huwa hawafanyi uchunguzi kama kiwanja utakachouziwa kinafaa kwa ujenzi. Unaponunua kiwanja cha namna hiyo bila kuwasiliana na mamlaka husika kuhakiki kama kiwanja ni halali kwa ujenzi ndiopale uwezekano wa kubomolewa unakiuwa mkubwa.

2.
Nyumba za Kupanga
Kama ilivyokuwa kwa viwanja vya kujenga, pia nyumba za kuapanga zinakuwa na matatizo kama hayo. Unakuta dalali anakupeleka sehemu ya kupanga nyumba au chumba huku akijua kabisa nyumba unayotakiwa kupanga kuna mkondo wa maji na imeshawekewa alama ya X kwa ajili ya kuvunjwa. Kwa kuwa madalali ya nyumba wanataka fedha za haraka hakufahamishi madhara ya kupanga nyumba hiyo. Matokeo yake inapita bomoa bomoa wakati hujamaliza hata mwezi wa kodi yako. 

Ili kuepuka hali hii isikutokee wakati unapotafuta nyumba ya kupanga, kiwanja cha kujenga au godown n.k, unashauriwa kuwatumia watalaam wa kupangisha nyumba ambao ni waaminifu na pale tatizo linapotokea katik nyumba yako au kiwanja wako tayari kuja kutatua tatizo hilo.

Tafadhali wasiliana na HOT EMI PROPERTIES kwa mahitaji yako ya nyumba, kiwanja, fremu, godown n.k bila kuhofia bomoa bomoa inayoendelea kwa simu na 0655 500 707 au email emayage@gmail.com

Usisahau kuchangia maada hii hapo chini. 

No comments:

Post a Comment