Kumekuwa na wimbi kubwa la matapeli katika biashara kuuza, kununua na kupangisha nyumba, viwanja, mashamba, fremu na magodown hapa Tanzania. Matapeli hao hutumia njia mbali mbali za utapeli. Leo nitaelezea njia tano tu ambazo hutumiwa na matapeli hao katika kuwaibia watu katika biashara ya Real Estates in Tanzania:
i. Kughushi Nyaraka za Umiliki
Hii ni njia ambayo hutumika sana katika utapeli wa mashamba, viwanja na nyumba. Kinachofanyika hapa ni matapeli kwa kushirikiana na watumishi wa umma wasio waaminifu, hughushi nyaraka zinazoonesha kuwa mali fulani inamilikiwa na mtu fulani. Kisha matapeli hao hutafuta mnunuzi wa mali hiyo huku wakiwasilisha nyaraka feki zinazoonesha umiliki wa mali hiyo.
ii. Kutumia Jeuri ya Fedha
Wakati mwingine mtu mwenye fedha anaweza kuamua kwenda kwenye kiwanja fulani ambacho siyo chake na kuamua kuanza kumwaga matofali, mchanga na kuanza kujenga. Hii ni dhuruma ambayo mwenye fedha huamini kuwa mkienda kwenye vyombo vya sheria atatumia fedha na atakushinda katika kupata haki yako. Na wakati mwingine huamini kuwa uamzi wa shauri hili utacheleweshwa hivyo yeye kuendelea kufaidika na mali hiyo ya dhuruma.
iii. Kupandisha Bei ya Mali Inayouzwa
Njia hii hasa hutumika na madali ambapo huongeza bei zaidi tofauti na mwenye nyumba, kiwanja au fremu anavyotaka. Wakati mwingine dalali anaweza kupandisha bei hata mara mbili ya ile bei mwenye mali aliyopanga kuuza au kupangisha mali yake. Hivyo ni bora unapofanya makubaliano na dalali wakati wa kufanya biashara ya real estates in Tanzania ujaribu kumuona na mwenye mali ili kuthibitisha uhalali wa bei iliyotajwa.
iv. Kuuziwa Eneo Lilotengwa Kwa Ajili ya Matumizi ya Umma
Hali hii hutokea pale ambapo matapeli huamua kumuuzia mtu eneo ambalo kisheria haliruhusiwi kuuzwa au kumilikiwa na mtu. Sehemu hizo inaweza kuwa viwanja vya michezo, maeneo ya kupumzika au ufukweni uliotengwa kwa matumizi ya umma. Utapeli huu pia unakwenda mbali zaidi pale mtu anapouziwa au kukodishwa nyumba au ufukwe wakati wa kiangazi, lakina masika yanapoanza eneo hilo hujaa maji na hivyo kushindwa kukalika.
Watu Wawili Kuuziwa au Kupangishwa Nyumba au Eneo Moja.
Utapeli wa namna hii hutokea pale dalali kwa tama yake huamua kuuza au kupangisha nyuma au eneo kwa watu wawili. Kila mmoja analipia kwa muda wake. Inapofikia hatua ya kuingia au kuendeleza eneo hilo wote wawili hukutana na kuonesha mikataba halali kabisa. Anapotafutwa dalali aliyesimamia mauzo au ukodishaji anakuwa hapatikani na simu inakuwa imefungwa kabisa.
Ili kuepuka utapeli wa namna hii na mwingine uluoko kwenye soko la real estates in Tanzania, ni vyema watu wakapata taarifa kamili na za kweli kuhusu kununua au kuuza nyumba, shamba n.k. Taarifa hizi unaweza kuzipata kutembelea ofisi za Hot Emi Properties Ltd zilizoko Sinza Kumekucha, Nyuma ya Deluxe Hotel.
No comments:
Post a Comment