Tanzania iko katika kipindi cha kampeni kumchagua Rais mpya wa awamu ya tano. Katika waliojitokeza na kupitishwa na vyama vyao na kisha kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni Ndugu Edward Lowassa na Ndugu John Pombe Magufuli.
Wagombea hawa wameanza kuhubiri sera zao kuhusu kuwaendeleza watanzania. Mambo yanayopewa kipaumbele ni kuondoa umasikini kwa wananchi. Nawaomba watanzania tuwahoji kuhusu ujenzi wa nyumba nafuu za watu wa kipato cha chini. Maana tukisema kuwa tukope benki tukakope nyumba zinazojengwa na taasisi mbalimbali kama NHC, Watumishi Housing, TBA na zingine binafsi, vipato vyetu haviruhusu kupata mikopo hiyo hivyo.
Ili kumaliza tatizo hilo, tuwahoji wagombea watatatuaji makazi duni ya maeneo ya manzese, Tandale, Tandika, na kwingineko ambapo watu wa kipato cha chini huishi kwa kuwajengea nyumba nzuri kwa bei nafuu.