Utakuwa umejionea jinsi sekta ya nyumba inavyokuwa ikidhihirishwa na ujenzi wa majumba mazuri jijini Dar es Salaam na mikoani.
Mashirika na makampuni kama NHC, TBA, Watumishi Housing Company, NSSF, LAPF GEPF na n.k wamejikita katika ujenzi wa majumba makubwa na kuuza kwa wananchi. Hali hii inatafasiriwa na watalaam wa real estates kuwa hapo baadaye bei za nyumba zinaweza kupungua. Hata hivyo hali inaonesha kuwa mahaitaji bado ni makubwa na nyumba zinazojengwa ni za bei kubwa kwa mwananchi wa kipato cha kawaida kuweza kuzimudu.
Hali hii inaleta sintofahamu kwa wale wenye nyumba za kupangisha za kawaida katika maeneo mbalimbali ya jiji na kwingineno wakihofia kuwa nyumba zao zitakosa wapangaji hapo baadaye. Lakini pamoja na hali ilivyo kwa sasa bado ujenzi wa nyumba za kawaida na fremu za maduka unaendelea kwa kasi ingawa katika maeneo mengine fremu bado zinakosa wapangaji.
Hatuhitaji kuacha kuendelea kujenga kuhofia kuwa nyumba zitakuwa nyingi. Haijawahi kutokea na wala haitatokea kuwa soko la nyumba likakosekana ingawa katika kiasi fulani linaweza kuyumba kama ilivyotokea Marekani na Ulaya.
Kwa wale wanaohitaji nyumba na viwanja kwa ajili ya ujenzi wasiache kututafuta ili kuwa dili nzuri. Au kwa wale wanaoendelea na ujenzi na wanataka mafundi bomba tuwasiliane kwa Dar City Plumbers
No comments:
Post a Comment